KITUI, Gavana Ngilu aungana na wafungwa kwa ibada maalum

0
1967
Gavana Ngilu akihutubia wafungwa katika jela kuu la Kitui baada ya ibada ya pamoja

Gavana wa jimbo la Kitui Bi. Charity Kaluki Ngilu hapo jana (Jumapili) aliunganika pamoja na wafungwa katika jela kuu la Kitui GK viungani mwa mji mkuu wa gatuzi hilo kwa ibada ya pamoja.Bi. Ngilu alitumia fursa hiyo kuwashauri kurekebisha tabia na mienendo yao ili wawe mfano wa kuigwa katika jamii.Aidha aliwahimiza wafungwa wanaotumikia kifungo chao kwa kupatikana na makosa tofauti tofauti kujihusisha na mafunzo yanayotolewa na idara ya mahakama nchini ili kupata ujuzi katika sekta mbalimbali kuwawezesha kujikimu pindi watakapoachiliwa huru.

Gavana Ngilu aungana na wafungwa katika jela la Kitui kwa ibada ya pamoja

Gavana Ngilu alielezea kufurahishwa kwake na mwenendo mwema wa kusifiwa baina ya wafungwa hao na kuwatia moyo wazidi kudumisha uhusiano mwema.Kiongozi huyo wa gatuzi aidha aliwapa motisha wafungwa hao na kuwaahidi kuwatembelea mara kwa mara kukagua jinsi wanavyopokea mafunzo katika taaluma tofauti kukuza uchumi wa taifa.Aliwapa changamoto kuhakikisha wamepata utaalamu katika nyanja tofauti ili kujikimu baada ya kutumikia kifungo chao.Aidha, Gavana Ngilu aliahidi kuwatembelea mara kwa mara kukagua jinsi wanavyopata mafunzo katika nyanja tofauti.

Hapo baadaye Ngilu aliunganika na waumini katika kanisa la Amazing Grace kwa ibada na mchango wa pamoja kusaidia kuendeleza upanuzi na ukamilishaji wa miradi iliyokwama kutokana na ukosefu wa fedha toshelevu.Aliwasifia waumini kwa mchango wao katika uongozi wake na kuapa kuwahudumia wakaazi wa Kitui kwa usawa bila kuegemea mrengo wowote wa kisiasa.

Bi. Ngilu akihutubia waumini katika kanisa la Katoliki Mbondoni, Mwingi

Baadaye, Bi. Ngilu alielekeza ziara yake katika kanisa Katoliki la Mbondoni, Mwingi Magharibi na hapo baadaye akaunganika na waumini katika kanisa la Katoliki Mwingi, eneo bunge la Mwingi ya Kati.

Facebook Comments Box