Uozo kufichuliwa katika Idara ya Utumishi wa Umma, Kitui

0
1557

Visa vya utovu wa nidhamu vimezidi kukithiri miongoni mwa watumishi wa umma na wasimamizi wakuu wa idara mbalimbali katika jimbo pana la Kitui kisa cha hivi punde kikihusisha naibu mkurugenzi mkuu katika idara ya Utumishi wa Umma Bwana Festus Malombe na mmoja wa wafanyakazi wa ngazi za chini katika idara hiyo.Mkurugenzi huyo ambaye pia ni mhubiri katika kanisa la Full Gospel Church almaarufu FGC eneo la Kathivo ameripotiwa kumdhalilisha na kumdhulumu Bi. Florence Wambua katika ofisi yake.

Bi. Wambua ni mtumishi wa umma katika serikali ya jimbo la Kitui na pia mi mwanafunzi katika chuo cha kadri cha Jubilee mjini Kitui.Kulingana na taarifa iliyofikia meza ya habari ya Kitui Online kutoka kwa mtumishi huyu wa serikali ya Kitui, mkuu wake kwa muda wa takriban miaka mitatu amekuwa akimshawishi kushiriki ngono jambo ambalo amekuwa akilikaidi.Amefichua zaidi kwamba watumishi wa kike katika idara hii wamekuwa wakipatia hali ngumu kwani mara kwa mara wamekuwa wakipata uhamisho kuhudumu katika sehemu za mbali na wanakotoka na hata wengine wao kupoteza nyadhifa zao za kazi kwa kukaidi agizo la Mkurugenzi huyu.

Florence Wambua amefichua bayana kwamba mkurugenzi msaidizi huyu anayefahamika kwa jina Bwana Festus Malombe amekuwa akimlazimisha kushiriki ngono tangia mwaka wa 2016 jambo ambalo lilizua uhasama baina yao.Nduru za kuamikika zimefichua kwamba baada ya ndoto ya mkuu huyo kukatizwa na ghafla na Bi. Wambua baada ya kuhitilafiana na wazo lake, alichukua hatua ya kumhamisha hadi sehemu za Endau/Malalani kama njia mojawapo ya kumuadhibu na kulipiza kisasi.Uhamisho wa Bi. Wambua kwa sasa umeidhinishwa na afisa mkuu msimamizi katika idara ya uhamisho jimbo la Kitui Bi. Clementine Munyithya.

Ripoti iliyotufikia ni kwamba kuanzia mwaka wa 2016 , Bwana Festus amekuwa akimualika Bi. Florence Wambua ofisini mwake na kumshawishi kuafikiana na agizo lake jambo ambalo amekuwa akilipinga vikali. Ni kutokana na msimamo mkali wa Florence mbele ya msimamizi wake uliomsababishia msururu wa vitisho na kuonywa kwamba katu hatakubalika kuikaribia ofisi ya mkuu huyo.

Kwa sasa Bi. Wambua anamrai Gavana wa Kitui Bi. Charity Kaluki Ngilu kuingilia kati haraka iwezekanavyo kuokoa watumishi wa kike katika serikali yake jinsi alivyoahidi wakati wa kampeni endapo angetwaa ushindi.Wito huu umetolewa kutokana na tetesi kutoka kwa baadhi ya watumishi kwamba wamekusudia visa vya unyanyasaji na vitendo vya kudhulumiwa na wafanyakazi wenzao wa kiume katika gatuzi la Kitui.Aidha anaitaka idara husika kutafuta mbinu mwafaka itakayomhakikishia usalama wake na wenzake wa kike katika sehemu zao za kazi.Bi.

Bi. Wambua pia ameweka bayana kwamba mwaka uliopita mkurugenzi huyo aliwatembelea ofisini mwao wanapofanyia kazi na kumsingizia kuwa mpotovu kimaadili na nidhamu kazini.Kilichofuatia ni kumkabidhi barua ikimhusisha kuwa na utovu wa nidhamu kazini.Baada ya kuripoti kisa hiki cha mkuu wake katika ofisi ya Katibu Mkuu wa jimbo la Kitui Bw. Alex Kimanzi, mkurugenzi huyu aliomba kusamehewa naye Bi. Wambua kwa wingi wa hamu ya kumsamehe akakubali kuzika tofauti baina yao.

Kinaya Ni kwamba baada ya kipindi kirefu mkurugenzi huyo anaonekana kurudia mwenendo wake potovu wa hapo awali jambo ambalo linaonekana kuwa kero na tishio kwa wafanyakazi was kike.

Facebook Comments Box