Kalonzo akerwa na Muungano, asambaratisha ndoa changa

0
1014
Wiper Leader Kalonzo Musyoka (left), Makueni Governor Kivutha Kibwana (centre), Sen. Mutula Kilonzo Junior (right) and others during Masongaleni Ward by-elections campaign. Photo/Standard

Kutokana na ongezeko la ugomvi kati ya kinara wa chama cha WIPER Dkt. Stephen Kalonzo Musyoka na Gavana wa Makueni Prof. Kivutha Kibwana, na ambao kwa muda umekua ukishuhudiwa hata mbele ya makutano ya umma, hali hii sasa imemlazimu Musyoka kuchukua hatua ya kuvunja uhusiano wa kisiasa uliotiwa sahihi na wawili hao kabla ya uchaguzi mkuu uliopita.

Kwa muda, wawili hao wamekuwa wakikabiliana vikali kwa kurushiana semi za maneno, licha ya kuwa Kibwana ndiye gavana aliyechaguliwa kwa tiketi ya Wiper katika majimbo matatu ya Ukambani, ambapo inakisiwa kwamba Kibwana ananuia kumyeyusha Musyoka, Jogoo wa Ukambani, asiweze kutimiza ndoto yake kuliongoza taifa 2022.

Hayo yalifichuka baada ya Kalonzo kumwandikia barua msajili wa vyama vya kisiasa nchini, huku akimweleza wazi kwamba hakuna mkataba baina ya vyama hivyo viwili, hivyo basi kila chama kiko huru kivyake licha ya kuwa wote ni wazawa wa eneo moja la Ukambani.

Pindi tu baada ya kuchaguliwa kwa kipindi chake cha pili, Kibwana alionekana kuchukua mkondo tofauti wa kisiasa huku akishtumiwa kukaidi maagizo ya Wiper, kwa mara moja sauti yake ilinaswa na kusambazwa kupitia vyombo vya habari huku akimtaka Makamu huyo wa zamani kustaafu katika siasa na kuiunga mkono ndoto yake kuingia ikulu 2022, hatua ambayo inahofiwa kutomfurahisha kamwe kiongozi wa Wiper pamoja na wafuasi wake.

ilumbi.kioko@gmail.com

Facebook Comments