Mwanaume afikishwa kizimbani kwa kosa la mauaji

0
707

Mwanaume mmoja mwenye umri wa makamo hii leo alifikishwa katika mahakama moja mjini Kitui kujibu mashtaka ya mauaji dhidi yake.Mshukiwa huyo kwa jina John Muatha David anashtakiwa kosa la kumuua kakaye wiki jana katika kijiji cha Kathambangii katika lokesheni ya Wikilikye, Kaunti Ndogo ya Kitui ya Kati.

Inadaiwa kwamba mshukiwa mwenye umri wa miaka 45 alimpiga hadi kumuua kakaye.Hata hivyo, mshukiwa alikana mashtaka dhidi yake mbele ya Hakimu Steven Mbungi.

Hakimu Mbugi aidha aliamrisha mshukiwa huyo kupelekwa Katika hospitali ya Mathare jijini Nairobi kufanyiwa uchunguzi wa kiakili kabla ya kusomewa tena mashtaka dhidi yake mnamo tarehe 19 mwezi huu.

Mwisho

Facebook Comments
ALSO READ:  KICOTEC Has Gulped Funds For Water,Health And Roads, Kitui MP