Serikali yasifia zoezi la sensa Ukambani

0
933

Huku zoezi la sensa likiendelea, serikali imedhihirisha kuridhishwa kwake na jinsi linavyoendesha kote nchni chini ya usimamizi wa wakuu kutoka vitengo tofauti serikalini.

Katika eneo la Ukambani linalojumuisha kaunti za Kitui, Machakos na Makueni, Katibu wa Wizara ya Ardhi Gideon Munga’ro alizuru kufuatilia jinsi zoezi hilo linavyoendeshwa.

Akizungumza Na wanahabari Jumanne nje ya ofisi ya kamishna wa kaunti ya Kitui, Mung’aro alisema hakujakuwa na ripoti zozote za utovu wa usalama na kuongeza Kuwa zoezi Hilo linaendelea Kwa usawa.

Aidha aliongeza Kuwa kupatikana Kwa idadi kamili ya wananchi wa Kenya kutasaidia serikali katika maswala ya ugavi wa fedha na raslimali katika maeneo tofauti hapa nchini.

Hata hivyo Mung’aro aliwapongeza wananchi pamoja Na afisa wa usalama Kwa kushirikiana Na maafisa wa kuhesabu watu kikamilifu na kudumisha usalama wakati wa zoezi hili linalotarajiwa kufika Kikomo mnamo tarehe 31 mwezi Huu.

Facebook Comments
ALSO READ:  Talanta lazima zikuzwe nchini, Musambi