Wakaazi wa Mutha waombwa warudi makwao

0
1543

Kamishna wa kaunti ya Kitui John Ondego amewaomba wakaaazi wa Mutha kitui kusini kurudi katika makaazi Yao kwani usalama wa eneo hilo umaimarishwa.

 

Kauli hii yake inajiri baada ya wakaazi hao kutoa lalama zao kuhusu utovu wa usalama ulioshuhudiwa sehemu hiyo majuma mawili yaliyopita kufuatia wafugaji wa ngamia wanaodaiwa kutokana Na jamii ya kisomali kutoka kaunti jirani ya Tana River.

 

Wenyeji hao walihofia Maisha Yao Na kutorokea vichakani huku wengine wakikita Kambi katika kituo cha polisi cha Mutha kwani walishaji Hao wa ngamia walikisha kimabavu Na kuwavamia  wenyeji hao wakiwa wamejihami Kwa bunduki.

 

Akizungumza Na wanahabari Leo Ondego amesema kuwa wameongeza afisaa wa usalama wanaoshika Doria usiku Na mchana eneo Hilo Na kwamba tayari wasomali Hao wamesharudi kwao hivyo kuwatakaka wakaaazi kutohofia kurudi makwao kwani usalama unaendelea kudumishwa eneo hilo.

 

Hata hivyo ameongeza kuwa eneo la Mutha Ni sehemu ya msitu Na uhifadhi wa wanyamapori hivyo hakuna Mtu yeyote anayeruhusiwa kuishi hapo.

 

Aidha amewahimiza wafugaji pamoja Na wenyeji wanaoishi sehemu hiyo kuhama kwani si Salama Kwa kuishi ikizingatiwa wanyama hatari wa porini pia wanaishi humo.

Facebook Comments Box