Nzige wateketeza maekari ya mashamba – Kitui

0
1877

Wakaazi wa jimbo la Kitui kwa sasa wanaililia serikali kuu kwa ushirikiano na ile ya kaunti kuwatafutia suluhu la kudumu kuwanasua katika mtego uliowatega maelfu ya wakulima hasa katika eneo la Mwingi.

Kwa muda wa takriban siku nane mfululizo, wadudu hao waharibifu wamezidi kuyakandamiza maelfu ya maekari ya mashamba huku njaa ikianza kuwakodolea macho kwani zao la mahindi ndilo tegemeo lao la kipekee kujikinga athari za njaa.

Katika mahojiano na Kitui Online, mmoja wa wakaazi wa Mwingi alifichua kwamba licha ya juhudi za serikali kupambana na wadudu hao waharibifu, mashamba yao bado yangali yanateketezwa na nzige.

Kwa sasa, wakaazi hao wanaitaka serikali kuu kutafuta suluhu la kudumu kuwakabili nzige hao kabla ya kusababisha uharibifu zaidi.

Kaunti ya Kitui ni miongoni mwa kaunti za hivi punde kuripotiwa kuvamiwa na wingu la nzige huku athari zake zikiwa si tu kwa mimea mashambani mbali pia lishe ya mifugo wao.

Kufikia sasa wadi 9 katika eneo la Mwingi zimeripotiwa kuathirika vikali kutokana na vamizi hilo.

ALSO READ:  Musila Unveils Kennedy Moki as his Running Mate

Baada ya kuripotiwa kwa kwa nzige hao, wizara ya Kilimo ilituma helikopta katika sehemu 3 ambazo zilikua zimeathirika kwa kiasi kikubwa, Ngomeni, Kivou na Kyuso.

“Punde tu shamba letu likipovamiwa na nzige,tulijitokeza kukabiliana na wadudu hao kwa kutumia chochote kile angalau kuiokoa mimea yetu.Tulitumia vijisehemu vya mabati huku wengine wakipiga mayowe na kupiga ngoma,” Alisimulia Kimanzi, mkulima kutoka Kaunti Ndogo ya Kyuso.

Wakulima hao ambao matumaini yao yameanza kupungua wanaiomba serikali kuingilia suala hilo kikamilifu na kuchukua hatua za kidharura kuwanusuru kutokana na janga hilo.

Uharibifu huo umeathiri pakubwa sehemu za Nguni, Kiomo, Kyethani, Thaana na Migwani.

Facebook Comments Box