Makueni yapakana na Taita Taveta Mto Tsavo, Bunge La Makueni Laamua

0
1015

Baadhi ya wawakilishi wadi katika gatuzi la Makueni hii leo wamezuru eneo tata katika wadi ya Mtito Andei, eneo bunge la Kibwezi Mashariki, linalozozaniwa na majimbo ya Makueni na Taita Taveta.

Kaunti hizi mbili zinaendeleza vita dhidi ya umilikaji wa Mtito Andei, mji maarufu sana katika barabara kuu inayounganisha miji ya Nairobi na Mombasa. Katika ziara hiyo ya ghafla, watunga sheria hao wa bunge la Makueni wameweka kibango katika Mto Tsavo kuashiria mpaka wa kaunti za Makueni na Taita Taveta.

A ssection of Makueni County Assembly

Hatua hiyo imechukuliwa siku chache baada ya afisa Katika afisi ya utozaji kodi katika kaunti ya Taita Taveta kuzuru mji huo ambao unaaminika kuwa kivutio cha utalii. Hii si mara ya kwanza kwa kaunti hizo kuzozania mji huo ambao umesheheni mahoteli ya kifahari ikizingatiwa kwamba hushuhudia idadi kubwa ya watalii wanaozuru mbuga la wanyama la Tsavo.

Hata hivyo, kibango hicho kiliondolewa na maafisa kutoka katika serikali ya kaunti ya Taita Taveta muda mchache baada ya kubandikwa.

Facebook Comments Box
ALSO READ:  Government asked to speed up reconstruction of Kavutini primary sch in Kitui East